December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kumjengea nyumba mama mjane wa mtoto Alhaji

Dkt. Samia kuwasomesha watoto wote 5 wa Mwanamama huyo.

Dkt. Samia kumpa Mwanamama huyo Mtaji wa Milioni 5 kwa biashara.

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ikiwa ni siku moja tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda kupokea changamoto ya kijana Alhaji Yahya Abdallah ambaye anafanya biashara ya kuuza ndizi kumsaidia Mama yake na wadogo zake 4 na Mwenezi Makonda kwa niaba ya CCM kumuahidi kumsomesha na Kumpatia kiasi cha Fedha kwaajili ya vitendea kazi na sare za shuleni.

Leo 4 Februari, 2024 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha kuguswa zaidi na jambo hilo na kumsaidia Mwanamama huyo mjane kwa kumpatia kiwanja na kumjenga Nyumba kubwa ya kuishi na watoto wake wote ambapo ujenzi wa nyumba hiyo utaanza Ijumaa tarehe 9 Februari, 2024.

Pia, Dkt. Samia kuwasomesha Watoto wote 5 wa Mwanamama huyo pamoja na kughariamiwa vifaa vyote vya shule na sare.

Aidha, Dkt. Samia amempatia Mwanamama huyo Kiasi cha Tsh Milioni 5 itakayokuwa inatolewa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigoma Mjini kwaajili ya kufanya shughuli zake za biashara kujikwamua kiuchumi.

Vilevile, Dkt. Samia kumgharamia Mwanamama huyo huduma ya Afya kwa kumagizia Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuhakikisha Mwanamama huyo mjane anafikishwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi wa tatizo alililonalo la uvinbe tumboni na kupatiwa matibabu.

Hayo yote yamewasilishwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda alipofika nyumbani kwa Mwanamama huyo mjane kumtembelea na kutoa salamu hizo za upendo kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.