November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kumaliza kero ya maji Same

Na David John,Timesmajiraonline, Kilimanjaro

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ametoa pongeze na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuleta Fedha nyingi zenye lengo la kuhakikisha Miradi yote inayotekelezwa ndani ya Wilaya hiyo inakamilika kwa wakati

Amesema Rais Dkt Samia amewafuta machozi wananchi wa same kwa kwakuweza kuleta ufumbuzi wa Maji na kuwahakikishia Wananchi wa wilaya ya Same kupata maji kwa kutokana na Miradi inayoendelea kutekelezwa na Ruwasa nakwamba mradi mkubwa wa Maji Mwanga Same korogwe ukiendelea kukamilika ambapo kwa hiyo wilaya ya Same umefikia asilimia 90

Kasilda ameyasema hayo Juni 1 mwaka huu wilayani humo ambapo amewaomba wananchi wote wa wilaya Same kuendelea kuunga juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa Kazi kubwa anayoifanya hapa Nchini na katika Wilaya hiyo miradi yote ya Same ikiwamo vituo vya Afya barabara za Tarura shule zinakamilika kwa wakati.

“Nawapa faraja sana wananchi wa Wilaya yetu ya same kwani rais.Dkt Samia ameweza kusikia kilio chenu cha uwepo wa changamoto ya Maji lakini hapa ninapoongea tayari sekali iliingia mkataba na mkandalasi Kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Maji wa mwanga same Korogwe na mradi umefikia asiliamia karibu 90 na unakwenda Kwa Kasi sana.”Amesema Kasilda

Amefafanua kuwa wananchi wenyewe wa Wilaya hiyo wanaona hata namna mabomba yalivyolazwa barabarani hiyo yote nikuashilia kwamba mradi unaendelea kutekelezwa mradi huo ni mkubwa sana katika Wilaya hiyo na mheshimiwa Rais Dkt .Samia ameamua kuwanusuru wananchi hao Kwa kilio hicho cha Maji na mkataba huo utatekelezwa Kwa miezi 14 tangu walivyofunga mkataba.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya Amesema kuwa licha ya mradi huo wa Maji lakini Rais Dkt Samia ameweza kuapelekea fedha Kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na Hospitali iliyopo Sasa ni muda mrefu ni chakavu na majengo yamechoka hayakidhi mahitaji Sasa Kwa wananchi wa samu wapatao zaidi ya laki tatu na sio idadi hiyo tu kwasababu Wilaya hiyo ipo barabara kuu hivyo idadi ya watu wanaopita ni kubwa.

Ameongeza kuwa Kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali hiyo imeshatengwa Bilioni mbili na hadi kukamilika Kwa mradi huo unagharimu shilingi Bilioni saba na sio Hospitali tu bali Kuna vituo vya afya tisa na Kati ya hivyo vituo sita vimekamilika na vitatu bado vinajengwa lakini pia Kuna miradi mingine ikiwamo jengo la dharula.