Na Penina Malundo ,timesmajira,Online
RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka Watetezi wa haki za binadamu nchini,kutetea kweli haki za binadamu , kuhimiza watu kufanyakazi kwa bidii na uwajibikaji ili haki hizo za binadamu zionekana kwa uwazi.
Rais Samia ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),amesema watetezi hao wanapaswa kutotetea haki za kisiasa bali watetee makundi ya watoto katika jamii ikiwemo wale wanaobakwa.
Amesema kuwa kazi ya kulinda haki ya mwanadamu inapaswa kufanywa na watu wote ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa sababu haki ya binadamu ni maendeleo na maendeleo ni kitovu kwa wanadamu.
“Kuheshimu haki za binadamu ni sehemu ya maendeleo ya nchi na Tanzania imekua na sera ya maendeleo iliyozingatia haki ya mwanadamu tangu mwaka 1967 tulipotangaza azimio la Arusha,”amesema na kuongeza
“Dhana nzima ya watetezi wa haki za binadamu mimi kama mwanadamu pia nakubaliana nayo,”amesisitiza
Amesema kutokana na matakwa ya tamko la umoja wa mataifa la watetezi wa haki za binadamu la 1998 na ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania serikali ina jukumu na ni mtetezi mkuu wa kulinda haki za kijamii haki za binadamu na haki za watu.
“Mtetezi mkubwa wa haki za binadamu ndani ya Tanzania ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo serikali ndio inatekeleza ndio sheria mama ambayo ina haki zote za wanadamu wanaoishi Tanzania,”amesema
Kwa upande wake Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa amesema wamezindua taarifa yao ambayo itaweka wazi kwa miaka 10 wamefanya nini na wanatarajia kufanya nini kwa miaka ijayo.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato