January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia awataka wana mbeya kuendelea kuliombea Taifa

Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya

RAIS Samia  Suluhu Hassan amewataka wana Mbeya kuendelea kuliombea Taifa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja viongozi kuendelea kusimamia usalama wa wananchi.

Mh.Rais  Samia amesema hayo leo wakati wa maandamano yaliyoambatana na matembezi ya hisani ya kumpongeza Rais yaliyoratibiwa  na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.

Rais Samia alipiga simu na kutoa salamu kwa wana Mbeya baada ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya kuhutubia wananchi katika viwanja  vya kumbukumbu ya Sokoine Mkoani hapa.

“Niwatakieni kila heri   kwenye maandamano na mikutano yenu  pamoja na kuendelea kuchunga usalama wa wananchi “amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema  kuwa wana mbeya wanakiri kwa vitendo  mambo makubwa aliyofanya  Rais Samia Suluhu Hassan  na Tanzani nzima.

 Homera alitaja baadhi ya miradi ikiwepo uwekezaji wa  Bil.22 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya afya ikiwemo  hospitali ya wilaya ya Igawilo  kwenye jengo la mama na mtoto ,jengo la upasuaji ,chumba cha  kutakasa  vifaa tiba,jengo la X -ray  pamoja na  vituo vya afya (8) katika mkoa wa Mbeya.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa  Rais Samia pia katika  kipindi ametoa Bil.68 kwa ajili ya  sekta ya elimu mkoani  mbeya.

Katibu mkuu umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa(UVCCM)Kenani Kihongosi amesema kuwa amefurahishwa na kuona mkoa wa Mbeya umefanya vizuri kwenye mikopo ya aslimia 10 ambayo inatolewa kwa vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu ambapo jumla  bilioni .2.6.

Pia Kihongosi aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia jumla ya shilingi Bil.570 zimetolewa kwenye mikopo ya elimu  ya juu kwa ajili ya kujikimu wanafunzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Mbeya Mchungaji Jakob Mwakasole amesema kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kuwarejesha wanafunzi 447 ambao walipata ujauzito wakiwa shule na wanaendelea na masomo.

Mwakasole ameeleza kuwa pia Rais Samia ameweza kutoa shilingi mil. 185 kwa ya ujenzi wa josho ili kuthibiti  magonjwa ya  mifugo ili  kuokoa mifugo  ili  isipatwe na magonjwa.