Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wasanii wa Sarakasi hapa nchini, Ibrahim na Fadi maarufu kama ‘Ramadhan Brothers’ kwa kuonesha ubunifu mkubwa katika kipindi cha GotTalentAU.
Akitoa pongezi hizo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amesema vijana hao wameitangaza vyema Tanzania na kuwatakia kheri katika muendelezo wa sanaa yao.
“Nawapongeza wanangu Ubrahim na Fadi (Ramadhani Brothers), kwa kipaji na ubunifu wenu wa kucheza Sarakasi.
“Onesho lenu lenu kupitia kipindi cha GotTalentAU,limeitangaza vyema nchi yetu ya Tanzania na nawatakia kheri katika kuendeleza sanaa yenu na kushiriki katika maonesho mbalimbali,” aliandika Rais Samia.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania