January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia awapa shavu wasanii, kulipwaDesemba 2021

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema malipo wanayostahili kulipwa Wasanii wa muziki hapa nchini kutokana na kazi zao kuchezwa kwenye Radio na TV mbalimbali za Tanzania pale kazi zao zinapotumika yataanza kutolewa December 2021 mwaka huu.

Akiongea na Vijana leo, kwenye uwanja wa Nyamagana Mwanza, alipokuwa kwenye ziara yake ya siku tatu Rais Samia amesema, ili kukuza sekta ya sanaa hapa nchini Serikali imeimarisha haki miliki za wasanii.

“Ili kuikuza sekta ya Sanaa Serikali tumeimarisha haki miliki za Wasanii, nataka kuwataarifu Vijana kuwa kuanzia December mwaka huu Wasanii wataanza kulipwa mirabaha yao kutokana na kazi zinazotumiwa kwenye radio, runinga au mitandaoni,” amesema Rais Samia.