December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia awakumbuka wanawake wa vicoba Kondoa.

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Oline

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Sh.milioni 10 kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake wa Vikundi mbalimbali vya vicoba wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariamu Ditopile alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua jitihada za wanawake nchini katika kazi wanazozifanya kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.

“Rais Dkt. Samia anawapenda sana wana Kondoa na wakati nakuja hapa niliwasiliana nae akanikabidhi Sh.Milioni 10 na amesema fedha hizo zikabidhiwe kwa vikundi vya vicoba zikawasaidie wanawake kujiimarisha kiuchumi”

Katika hatua nyingine Ditopile aliahidi kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kumkomboa mwanamke kiuchumi kwa kuwachangia Sh.Milioni Tano.