Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Bukoba
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,amewaagiza viongozi wote na wasaidizi kwa kushirikiana Wabunge kusimamia matumizi ya fedha kwenye maeneo yao.
Alitoa maagizo hayo Mkoani Kagera kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani humo.
Alisema Serikali itaendelea kutoa fedha kwaajili ya miradi muhimu ya maendeleo ya wananchi.
“Nitafanya kazi zaidi ili wananchi Mambo yao yakae vizuri kwa mustakabali wa taifa letu, napenda kujituma ili malengo ya wananchi yaweze kutumia”alisema Rais Samia Suluhu Hassan.
Alisema Serikali itaendelea kutoa fedha Kama ilivyohaidi kwaaji ya kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi ( CCM ).
Awali mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali Charles Mbunge ,wakati alitoa taarifa kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alisema maelekezo yaliyotolewa na waziri mkuu Kassim Majaliwa,zao la kahawa lipande bei limefanikiwa.
Meja jenerali Mbunge,alisema maelekezo hayo yamefanikiwa kwa beia ya kahawa kupanda kwa asilimia 248 .
Alisema mnada wa kwanza umefanyika Wilayani Ngara Mkoani humo kahawa ya Arabika imeuzwa kwa shilingi ( 3,720) kwa kilo wakati mwaka Jana kilo moja ya kahawa hizo iliuzwa shilingi ( 1,500).
Waziri wa kilimo Hussein Bashe, alisema wakulima wa zao la kahawa waliteseka Sana miaka iliyopita Bei walikuwa wanapangiwa na viongozi wa ( AMCOSS).
alisema wakulima walikuwa na tozo 47 zikiwemo tizo ya burudani ya mwenyekiti .
Alisema wizara imeondoa mfumo kiritimba wa viongozi wa vyama vya ushirika kujimilikisha Mali za wakulima.
Alisema kulikuwa na biashara ya butura iliyokuwa ikijenga utaratibu wa kumdhoofisha mkulima wa Kahawa asipate faida na kilimo chake.
Alisema kwa Sasa kahawa za mkulima zinauzwa kwa njia ya mnada wa wazi na mkulima asiporidhika na bei hauzi kahawa zake.
Alisema tozo zote zinazotakiwa kulipwa sio jukumu la mkulima ni jukumu la mnunuzi.
Alisema mnada wa kwanza uliofanyika Wilaya ya Ngara kwa Mara ya kwanza kahawa ya Arabika imeuzwa shilingi (3,720).
Alisema baada ya mnada huo kufanyika ametoa maelekezo wakulima walipwe fedha zao ndani ya masaa 24.
Alisema pia mwaka Jana wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wataalam wa kilimo na wadau wa Kahawa waligawa bure miche milioni 3 ya kahawa bure kwa wakulima.
Alisema mwaka huu wanatarajia kugawa Miche Milioni 20 kwa wakulima bure bila malipo ili wananchi waweze kuboresha zao la kahawa ambalo lilikuwa limeanza kutelekezwa.
Hata hivyo aliwaelekeza wataalam wa kilimo wanaohusika na ugawaji wa Miche hiyo kuwapa wakulima Miche kuanzia (1,500) ndio itaonyesha matunda ya Kilimo Cha zao Hilo sio kuwapatia Miche 5 ambayo haitakuwa na faida kwa mkulima.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini