December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia ateua wenyeviti

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Juni, 2021 amefanya uteuzi wa Wenyeviti wanne (4) wa  Bodi za Wakurugenzi kama ifuatavyo:-

  1. Amemteua Dkt. Fenella Ephraim Mukangara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Dkt. Mukangara  ni Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  2. Amemteua Brig. ( Mstaafu) Aloyce Damian Mwanjile kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania.
  3. Amemteua Bw. Khalfan Ramadhani Khalfan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
  • Amemteua Capt. Mussa Mandia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).

Uteuzi huo unaanza leo tarehe 19 Juni, 2021.