Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza Baraza la Mawaziri,huku akimteua Jumaa Aweso na Mhandisi Kundo Mathew kwa mara nyingine kuongoza Wizara ya Maji.
Akitangaza baraza hilo Novemba 17,2025 Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Rais Dkt.Samia ameunda Wizara 27 na kuteua Mawaziri 27 na Manaibu Mawaziri 29, ambapo amemteua kwa mara nyingine Jumaa Aweso kushika nafasi ya Waziri wa Maji huku Mhandisi Mathew Kundo kushika nafasi Naibu Waziri wa Wizara hiyo.
Pia Dkt.Samia amewateu kwa mara nyingine Abdallah Ulega kuwa Waziri wa Ujenzi na Mhandisi Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo pamoja na Profesa Kitila Mkumbo kuendelea kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji.
Mwingine ni Dkt.Doroth Gwajima ambaye ameteuliwa kwa mara nyingine kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,huku katika Wizara ya Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akiendelea kuongoza Wizara hiyo kwa mara nyingine.
Sanjari na hayo Dkt.Samia katika Wizara ya Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amemteua Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri huku Naibu Waziri ni Regina Qwaray.
Ofisi ya Rais -Maendeleo ya Vijana
Waziri ni Joel Nanauka huku Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Waziri ni Mhandisi Hamad Masauni na Naibu Waziri ni Dkt. Festo Dugange
Hata hivyo Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu ni Waziri William Lukuvi huku Naibu Waziri: ni Ummy Nderiananga.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako