December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia apongezwa kwa mageuzi kwenye uwekezaji

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan, imepongezwa kwa namna inavyofanya mageuzi katika sekta mbalimbali hususani ufanyaji biashara kwenye uwekezaji hatua ambayo imeendelea kuwavutia wawekezaji duniani kuja kuwekeza  Tanzania.

Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya washiriki kwa nyakati tofauti kwenye hafla  ya kufunga maonesho ya 25  kimataifa ya ujenzi .

Mkurugenzi Mwenza wa Nazneen Material Holding Company, Hafeezal Gangji, akizungumza kwenye maonesho hayo  alisema kuwa mazingira wekezaji yaliyopo hapa nchini ni bora na  na wamekuwa katika biashara ya tasnia ya vifaa vya nyenzo ya umeme kwa zaidi ya miaka 20.

Alisema wamekuwa katika tasnia ya wakisambaza vifaa vya kushughulikia nyenzo za umeme.

"Ushirikiano tuliopata kutoka katika kampuni za nje ya nchi  hii yote ni kutokana na uzoefu wetu katika tasnia ya kusambaza  vifaa vya kushughulikia nyezo za umeme," alisema Gangji.

Aidha , Mkurugenza Mwenza huyo alisema kuwa mbali na kampuni yake kuuza mashine za ujenzi pia wanakodisha mashine hizo kwa Taasisi na kampuni zenye miradi mikubwa.

"Hivi karibuni moja ya kampuni ya hapa nchini ilinununua nyenzo mpya ya kushughulikia umeme ya GODREJ kutoka kwetu kwa kuwa tumekuwa tukitegemewa katika huduma ya biashara hii kwa miaka zaidi ya 20 na tumekuwa tukishughulikia  nyenzo za umeme.

Kuja kwa mashine hizi mpya ni kiashiria cha mabadiliko madhubuti kuelekea kupata Suluhu endelevu kwa kutumia teknolojia hiyo mpya na rafiki kwa mazingira na kuuza uvumbuzi ndani ya sekta ya vifaa na huku ikiongoza njia kuelekea mustakabali endelevu zaidi," alisema Mkurugenzi Mwenza.

Kwa upande wake Meneja Ugavi wa Kampuni ya Karimjee, Sandeep Gambhir, alisema kampuni yao imepiga hatua kwa kununua mashine hiyo kwa kuelekea kufanya shughuli zake kuwa za kisasa.

"Tumekuwa tukitumia vifaa vya umeme vya GODREJ kwa miaka minne sasa na imethibitika kuwa ni ya kuaminima na rafiki wa mazingira na pia inaokoa gharama,"alisema Gambhir.

Aidha, washiriki wengine wa maonesho hayo walisema kuwa maonesho hayo yalikuwa na tija kubwa kufuatia washiriki hao kupata wabia wapya wa kushirikiana katika ufanyaji biashara.