Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
Mratibu wa Jukwaa la Usimamizi wa Unternal Tanzania (IGF)Dkt.Nazar Kirama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mkutano wa mtandao nchi za Afrika wa masuala ya intaneti kufanyika Tanzania.
Dkt. Kirama ,amesema hayo jijini hapa Mei 31,2025 katika mkutano wa 14 wa nchi za Afrika kuhusiana na masuala ya intaneti katika ukumbi wa mwalimu Nyerere.
“Jukwaa la usimamizi wa Unternal Tanzania tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu nchi yetu kupewa heshima katika mkutano wa masuala ya intaneti kwa nchi za Afrika “amesema Dkt.Kirama.
Dkt.Kirama amesema kufanyika kwa mkutano huo hapa nchini unatokana na mkutano wa awali uliofanyika nchini Uswizi.
Amesema kulikuwa na majadiliano mazuri awali katika mkutano wa wabunge wa Afrika kutoka jukwaa hilo ambalo linajumuisha wadau mbalimbali wanaoshiriki katika sera za nchi moja moja na kuleta mafanikio .
Aidha amesema kupitia mkutano huo utakuza sekta ya uchumi katika masuala ya intaneti na mfumo wa TEHAMA ambapo vijana wakitumia vizuri kupitia simu janja na YouTube chanel wataweza kupata kipato ajira na kuongezeka.
More Stories
CCM kusimamia kitabu cha Hayati Songambele kiingie mtaani
Mwendokasi kuendeshwa na ENG kwa miaka 12
Vitongoji 284 Arumeru Mashariki vyafikiwa na umeme