Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amekuwa miongoni mwa viongozi wa kitaifa walioguswa na kifo cha msanii maarufu nchini Grace Mapunda maarufu ‘Tesa’.
Kutokana na kuguswa na kifo hicho, Rais Samia alitoa salamu za rambirambi ambapo, Tesa alipoteza maisha Novemba 2 mwaka huu, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Akitoa salamu za pole kupitia ukurasa wake wa instagram, Rais Samia alisema; “Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wasanii hasa waigizaji wa filamu nchini kwa kuondokewa na ndugu yetu, Grace Mapunda.
“Kwa zaidi ya miaka 20 Grace ametumia kipaji chake kutupa burudani na kuelimisha mamilioni ya Watanzania kupitia tamthilia alizoshiriki. Mwenyezi Mungu ampumzishe pema na aendelee kuijalia familia yake faraja na subra,” aliandika Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
More Stories
Waziri Mkenda aeleza Tanzania ilivyoweka mikakati madhubuti Teknolojia ya Akili Unde
Polisi Mbeya yajivunia miaka minne ya mafanikio
Wahariri wa vyombo vya habari nchini wapongezwa