January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia ahutubia zaidi ya wananchi 30,000 waliofurika uwanja wa majimaji Songea Ruvuma

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan jana September 28,2024 amehitimisha Ziara yake ya Kikazi Mkoa wa Ruvuma kwa kuhutubia Maelfu ya Wananchi waliofurika Uwanja wa Majimaji Songea kwenye Mkutano wa hadhara wa kuagana na Wananchi wa Mkoa huo.

Rais Dkt. Samia amesema Ziara yake Mkoani humo iliyoanza September 23,2024 imekuwa na mafanikio Makubwa ambapo alitembelea Wilaya zote za Mkoa huo na kujionea namna fedha alizoleta zinatumika kutatua kero za Wananchi.

Aidha Rais Samia amewaahidi Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuwa Serikali itaendelea kuleta fedha za kutekeleza Miradi ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na kusimama kikamilifu Miradi inayoendelea Sasa ikamilike kwa wakati.