December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amesema usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo umeendelea kumpa faraja Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri Ndejembi alisema hayo juzi katika ziara yake maalum ya kimkakati ya siku ya pili katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne vilivyotengewa Sh milioni 98 nakubaki Sh milioni 17.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Annamringi Macha alisema madarasa hivi sasa miundombinu yake ni mizuri haijalishi iko vijijini au mjini.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita alisema Serikali imeanza mkakati ya kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu kila shule za msingi na sekondari.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mabala Mlolwa amesema juhudi za Serikali kuleta fedha zimefanya wananchi kutochangishwa Kama zamani fedha za Maendeleo ya mradi kwani walikuwa wakichangisha hata miaka mitatu mradi haukamiliki.

Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Mapamba, Rahel Wilson amesema ujenzi huo ulianza mwezi Julai ,2024 nakukamilika mwezi Oktoba mwaka 2024 .

“Ujenzi huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na msongamano wa wanafunzi changamoto iliyopo hakuna jengo la utawala,nyumba za walimu na maabara,” ali.sema Wilso