Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Eleuther Alphonce Mwageni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Prof. Mwageni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na anachukua nafasi ya Prof. Esther Ishengoma ambaye amemaliza muda wake.Uteuzi huu umeanza jana tarehe 07 Juni, 2021.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Neema Bhoke Mwita kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal).
Dkt. Mwita amechukua nafasi ya Dkt. Theodora Nemboyao Mwenegoha ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.Uteuzi huu umeanza leo Juni 8, 2021.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote