January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia ana kwa ana na wafanyabiashara

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti Mtendaji wa PMM Group Dkt. Judith Mhina Spendi kuhusiana na masuala mbalimbali ya Kibiashara wakati akielekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti Mtendaji wa PMM Group Dkt. Judith Mhina Spendi kuhusiana na Mafanikio pamoja na changamoto mbalimbali anazokutana nazo katika Biashara wakati akielekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa State Oil Group Bw. Nilesh Suchak kuhusu changamoto mbalimbali katika Biashara ya Mafuta wakati akiwa njiani kuelekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Bw. Elias Lukumay kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo pamoja na Mafanikio katika Sekta ya usafirishaji wakati akiwa njiani kuelekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Group Six Bw. Janson Huang kuhusiana na Uwekezaji ambao Kampuni hiyo imefanya wakati akiwa njiani kuelekea Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.