Aweka jiwe la msingi, alisisitiza umuhimu wa bandari hiyo
katika kukuza uchumi wa eneo hilo na Malawi, Msumbiji
Na Cresensia Kapinga, Timesmajiraonline, Nyasa
SERIKALI ya Awamu wa Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, imezidi kuimarisha miundombinu ya usafirishaji, safari hii ikiwa imetenga sh. bilioni 80 kwa ajiri ya ujenzi wa Bandari mpya Bambabay itakayojengwa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Katika mwendelezo wa kutimiza dhamira yake hiyo jana Rais Samia aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo mpya ambayo inaenda kukuza maendeleo endelevu baina ya Tanzania na nchi jirani za Msumbiji na Malawi.
Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wilaya Nyasa, mkoani Ruvuma, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa bandari hiyo katika kukuza uchumi wa eneo hilo na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za ndani na nje.
Rais Samia alisema bandari hiyo itawawezesha wakazi wa Nyasa kupata fursa za biashara, kuongeza ajira na kuboresha huduma za kijamii.
Ujenzi wa bandari hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha miundombinu ya usafirishaji nchini na kuonesha dhamira ya Rais Samia katika kukuza maendeleo endelevu nchini na nchi jirani ya Msumbiji na Malawi.
“Bandari hii itarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa nje na ndani hivyo niwaombe kuhakikisha bandari hii inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa lakini pia tuwe na miundo mbinu bora ya kupokea mizigo na bandari yetu kule Nkatabei nchini Malawi,” alisema.
Alisema dipolamsia ya kiuchumi sio bandari peke yake hata reli ya SGR nayo pia ni diplamasia ya uchumi.
Aliahidi kuwa Serikali itatoa msaada wa kutosha ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
” Nawashukuru wananchi wa Nyasa kwa mapokezi mazuri mliyonipa nipo hapa mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi na leo ni siku ya tatu ya ziara yangu yenye lengo la kugagua ,kuzindua na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokamilika na ambayo bado inaendelea kukamilisha,pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwa pamoja.” Alisema.
“Ziara yangu hapa Nyasa nimefanya vitu vikubwa viwili, kwanza nimezindua Barabara yenye urefu wa kilomita 66 ambayo imegharimu kiasi cha sh. Bilioni 112..76.
Shukrani za pekee ziwaendee wenzetu wa Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB) kwa kutusaidia fedha za kukamilisha ujenzi wa Barabara hii pia wamesaidia ujenzi wa reli ya SGR kule Kigoma,”alisema alisema na kuongeza;
“Uwepo wa Barabara hiyo umeleta faraja kubwa na unaenda kurahisisha usafiri wa watu na usafirishaji wa bidhaa niwaombe ndugu zangu kutumika barabara hii kuleta maendeleo na madereva watakaoitunia watumie kwa umakini ili kuepusha ajali.”
Kwa upande wake Waziri wa miundombinu, Inocent Bashungwa alishukuru Rais Samia kwa kuzindua Barabara yenye urefu wa kilometa 66.
“Na leo umeunganisha Bandari ya Mtwara na Bandari ya Nyasa kwa kutengeneza Barabara ya Mtwara corridor,” alisema Rais Samia .
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa ADB, Dkt. Patricia Laveri, Alisema matokeo hayo sehemu ya urafiki wa benki hiyo na Tanzania na kwamba kukamilika kwa Barabara ni tsehemu ya urafiki.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote