November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia aalikwa Vatican na Papa Francis

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Kufuatia mualiko wa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani na nchi ya Vatican Papa Francis, Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kitaifa Februari 11 hadi 12 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema lengo la ziara hiyo ni kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican.

Tanzania na Vatican tangu mwaka wa 1960 zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya amani, kiroho,elimu na afya.

“Kanisa Katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, za msingi 147 na za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110 pamoja na vyuo vikuu 5,” inaeleza taarifa iliyotolewa na wizara huku takribani taasisi za afya 473 zikiendeshwa na Kanisa Katoliki.

Tofauti za udini hazijawafanya viongozi hawa kushindwa kukaa pamoja na kujadili maslahi ya wananchi na uendelezaji wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.