Na Joyce Kasiki,Timesmajira,Dodoma
RAIS wa Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu yatakayoanza Mei 15 hadi Mei 20 mwaka huu mkoani Dodoma.
Aidha Maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi Mei 16 mwaka huu huku yakitarajiwa kuhitimishwa mnamo Mei 20 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema, maonyesho hayo pamoja na mambo mengine yataambana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi ,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) na semina itakayolenga kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wabunifu.
Amesema maonyesho hayo yanatoa fursa kwa wabunifu na wagunduzi kuonyesha Kazi zao kwa wadau na wanunuzi wa bidhaa wanazozitengeneza.
Aidha Profesa Mkenda amesema licha ya Mashindano hayo kufanyika kitaifa mkoani Dodoma lakini maadhimisho hayo yamefanyika kwa ngazi ya mikoa tangu April 27 Mwaka huu na yanatarajiwa kuhitimishwa Mei 14 mwaka huu.
Profesa Mkenda ametumia nafasi hiyo kuwaasa wadau na watanzania kwa ujumla kupenda na kununua bidhaa zinazobuniwa na kutengezwa kupitia wabunifu hapa nchini.
More Stories
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania