Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Februry 29,2024 saa 11:30 Jioni katika Hospitali Mzena Jijini Dar es salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu kwa ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.
Akitangaza msiba huo, Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Mzee Mwinyi alikuwa akipatiwa matibabu tangu November 2023 London Uingereza na baadaye kurejea Nchini na kuendelea na matibabu Hospitali ya Mzena.
Marehemu Mwinyi anatarajiwa kuzikwa Machi 2, 2024 visiwani Zanzibar, ambapo Bendera zitasimama nusu mlingoti kwa muda wa siku saba.
Mzee Mwinyi alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia Januari 30, 1984 mpaka October 24, 1985, alikuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania kuanzia mwaka 1985 mpaka 1995.
Hata hivyo, Mzee Mwinyi akiwa Rais wa Tanzania ndipo nchi nyingi barani Afrika ziliingia katika mfumo wa Vyama vingi vya siasa “Multiparty Democracy” hapo ndipo jina la utani la “Mzee Rukhsa” lilipoanza, kwani Serikali ilianza kuruhusu mambo mengi kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania pamoja na kukuza uhusiano na mataifa ya Magharibi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua