December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Picha ya Maktaba

Rais Magufuli mgeni rasmi Mkutano Mkuu Chama cha Walimu Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kesho Ijumaa atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Mkutano huo utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma huku watu wote wakitakiwa kuzingatia na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 wakati wa tukio hilo.