RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka watendaji ndani ya serikali kujiamini katika nafasi zao kwa kuchapa kazi na kuhacha dhana ya kila serikali mpya inapoingia madarakani panatokea mabadiliko.
Rais Magufuli ametoa wito huo leo Jijini Dodoma wakati wa kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi.
Rais Magufuli amesema kuwa mabadiliko yatakayokuwepo ni kwenye nafasi za uwaziri kwani wapo watakaorudi na wengine hawata rudi.
“Tena siku hizi chaguo ni kubwa, nina wabunge 264 kwa hiyo uchaguzi ni mkubwa Zaidi sitaki kusema uongo”, amesisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema watendaji hao wachape kazi wasiwe na wasi wasi, hakuna mabadiliko kwani walianza wote na watamaliza wote.
“Yani Nianze kuapisha tena wakuu wa mikoa 26 siwezi, hata kuapisha kunachosha watabaki wale wale labda watakao staafu au kuwa na utendaji mbovu”, amesema Rais Magufuli.
“Wakuu wa mikoa na wilaya naona wanakuwa na hofu na washangaa kwanini wanapata hofu maana kama mafanikio ya serikali ni pamoja na wao, kama ni ushindi wangu wa asilimia 84.4 umechangiwa na wao kwa kazi nzuri waliofanya kwa miaka mitano, wasi wasi wanini! Ameshangaa Rais Magufuli.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati