LUSAKA, Rais wa Zambia, Edgar Lungu ameanguka akiwa katika maadhimisho ya 45 ya Siku ya Ulinzi Kitaifa nchini humo baada ya kupata kizunguzungu cha ghafla.
Lungu alianguka juzi ambapo alilazimika kusitisha kila kitu na kurejea ofisini kwake katika Ikulu iliyopo mjini Lusaka ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo.
Tukio la aina hiyo ni la mara ya pili kwani Mei 8, mwaka 2015 Rais Lungu alianguka tena kutokana na hali inayofanana na hiyo.
Katibu wa Baraza la Mawaziri, Dkt.Simon Miti alisema kuwa,baada ya hali hiyo Rais Lungu alilazimika kurejea Ikulu na afya yake inaendelea vizuri.
“Rais wa Jamhuri ya Zambia,Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu, mchana wa leo (juzi) amejikuta katika hali ya kizunguzungu akiwa katika maadhimisho ya 45 ya Siku ya Ulinzi Kitaifa. Hali ya Mheshimiwa Rais ilirejea vizuri haraka na kuelekea katika gari lake kurejea katika makazi yake kule Ikulu,”amesema Dkt.Miti.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria