Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam
RAIS Samia Suluhu Hassan ametengaza kufuta tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara vyama vya siasa ambapo kuanzia sasa ni ruksa kufanya mikutano hiyo.
Rais Samia ametangaza kufuta tangazo hilo Ikulu, jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na viongozi wa vyama 19 vyenye usajili.
“Mikutano ya vyama vya siasa ni haki ya vyama vya siasa. Uwepo wangu hapa leo ni kuja kutangaza kuwa lile tangazo la kuzuia ile mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa,” alisema Rais Samia na kushangiliwa na viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuriwa mkutano huo na kuongeza’
“Nina sema mikutano ya hadhara ni haki kwa vyama vya siasa, lakini ni jukumu lenu kuendesha mikutano ya hadhara kwa mujibu wa sheria.
Kwa upamnde wa Serikali wajibu wetu ni kulinda mikutano ya vyama vya siasa mnatoa taarifa na kwa hatua tuliyofikia wajibu wetu ni kuwalinda.
Wajibu wenu vyama vya siasa nikufuata sheria na kanuni zinavyosema na kama Watanzania tunatoa ruhusa za mikutano ya vyama vya siasa tukafanye siasa za kujenga na sio kubomoa. Tukafanye siasa za kistaarabu. Sisi ndani ya CCM tunaamini kukosoa na kukosolewa.”
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi