November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikaii yafurahia mwenendo mzuri PUMA

Na Mwandishi Wetu  Dar es Salaam 

SERIKALI imesema inafurahishwa na mwenendo mzru wa kampuni ya mafuta, gesi na vilainishi na Puma Energy Tanzania katika biashara na ubunifu mbalimbali.

Miongoni mwa ubunifu huo ni pamoja na kuwatambua na kutoa zawadi kwa waendeshaji bora wa vituo vya mafuta vilivyo chini ya kampuni hiyo nchi nzima ambao wanafanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali ya utoaji wa huduma na bidhaa za Puma Energy.

Hayo yameelezwa jana Oktoba 20, 2023 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa NIshati Judith Kapinga, katika hafla ya kufunga mafunzo, kuwatambua, kuwatangaza na kuwapa zawadi waendeshaji  bora wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini.

Amesema huduma bora ndizo zinazoifanya 

kampuni hiyo iendelee kuwa namba moja kwa utoaji wa huduma za mafuta nchini, hivyo itaendelea kuiunga mkono kuhakikisha inaendelea kuwa katika ubora unaitakiwa na kuiletea nchi mapato zaidi.

Naibu Waziri Judith amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Puma Energy Tanzani ni kiongozi wa soko katika usambazaji na uuzaji wa bidhaa za mafuta ya petrol nchini.

Kwa mujibu wa Judith, kutokana na ubora wake imeendelea kuaminiwa kutoa huduma za mafuta katika miradi mingi ya kimkakati ya serikali ukiwamo ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere na mradi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).

“Hivyo nakupeni hamasa ya kuendelea kuchangamkia fursa hizo ambazo kipekee zinachangizawa na utayari wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

AITAKA KUFIKA VIJIJINI

Pamoja na pongeza lhizo, ameitaja kampuni hiyo kuendelea kupanua wigo wa ujenzi wa vituo vya mafuta hususan katika maeneo ya pembezoni.

“Licha ya kuwa na jumla ya vituo 74 Kwa nchi nzima lakini ukiangalia ukubwa wa kampuni hii vituo hivyo ni idadi ndogo sana, ongezeni juhudi na kujenga vituo katika sehemu mbalimbali za nchi hususan vijijini.

“Mnafahamu kuwa mafuta ni changamoto katika baadhi ya maeneo watu wanabeba madumu, hivyo tunawapa shime kuendelea kuongeza vituo. Najua mmesema kwamba mmeongeza vituo viwili lakini ningependa mwende mbele na mbele zaidi hususan kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa mkalete tija kubwa zaidi,” amesema.

MKURUGENZI MKUU PUMA

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdalla Amesema mafanikio ya kampuni hiyo yanatokana na kazi nzuri inayofanywa na watoa huduma wao waliopo katika vituo mbalimbali nchini.

Amesema wamekuwa wakiwapatia wateja wao huduma iliyobora kila wanapotembela vituoni, hivyo watoa huduma hao ndilo jicho la kampuni hiyo.

Amesema lengo la kampuni hiyo ni kuwapa huduma bora Watanzania kufikia malengo yao katika maisha hivyo wataendelea kuboresha huduma kulingana na wakati na mahitaji.

 Katika tuzo hizo Kituo cha Mafuta Cha Puma Arusha kiliibuka mshindi wa kwanza huku Puma Upanga ikitwaa nafasi pili kwa huduma bora.

Hafla hiyo pia ilihudhuliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Dk. Seleman Majige ambaye katika salamu zake aliahidi kumfanyia kazi maelekezo ya serikali yaliyotolewa na naibu waziri Judith kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo.