December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais aunda Kamati kutathminni utendaji Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda
Kamati kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza malengo ya
Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.
Ili kutekeleza azma hiyo amemteua Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa
Tanzania nchini Zambia kuwa Mwenyekiti wa Kamati. Aidha, amewateua wafuatao
kuwa wajumbe wa Kamati:

1) Balozi Ramadhan Mwombe Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu
Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu;

2) Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza;

3) Balozi Peter Allan Kallaghe, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

4) Balozi Tovako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 31 Machi, 2023 Ikulu Dar es Salaam, saa
08:30 mchana.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu