Na Mwandishi wetu , TimesMajira Online
Mtoto Rafat Ally Simba ambaye hivi karibuni alitikisa vyombo mbalimbali vya habari nchini baada kuandika na kuzindua kitabu chake cha The First Female President, yaani Rais wa Kwanza Mwanamke sasa ameibukia Chama Cha Mapinduzi CCM na safari hii akiwania nafasi za Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Chipukizi Taifa Bara na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa.
Kwa mujibu wa UVCCM, jina la Rafat mwenye miaka 11 ambaye pia mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji ya Chipukizi Tawi la Boko limerudi likiwa nafasi ya pili jambo linalomuhamasisha Mwanachipukizi huyo ambaye pia ni msemaji wa hadhara, yaani motivational public speaker, kutumia uwezo wake katika kuhamasisha watoto na vijana wenzake kujitambua, kujiamini na kupigania ndoto zao.
Kwa sasa Rafat Ally Simba ni mwanafunzi wa Darasa la sita katika shule ya Msingi Turkish Maarif iliyopo wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es salaam akihudumu kama kiongozi mkuu wa wanafunzi shuleni hapo.
Kariba ya kiungozi kwa mtoto Rafat ipo kwa damu ambapo mbali na masomo Binti huyo ni mwana mazingira, ambaye anaamini kuwa maisha ya usoni hasa kwa watoto yatategemea sana ni jinsi gani mazingira yanatunzwa kwa sasa.
“Hatuwezi kufikiria kuwa viongozi wa kesho iwapo kesho hiyo haitakuwa salama, hivyo nahamasisha vijana wenzagu kujitambua, kujiamini na kupigania ndoto zetu,” amesema mtoto Rafat Ally Simba.
Kwa upande wa lugha, Rafat anazungumza lugha tatu ikiwemo Kiswahili, Kiingereza na kifaransa emesema ufahamu wa lugha ni muhimu sana kwa kiongozi katika kuwasiliana na watu wake kwa ufasaha
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi