June 14, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rabia: CCM inathamini kila jasho la Mtanzania

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Lindi

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdalla Hamid, amesema Chama cha Mapinduzi kina thamini jasho la kila mtanzania, hivyo serikali ya CCM itakikisha kila kundi la kijamii linaguswa ilikuhakikisha linafanikiwa na shughuli zote za kujitafutia mali sambamba na huduma zote zinatokana na Serikali.

Rabia ameyasema hayo leo Juni 14, 2026 Mkoani Lindi alipo kutana na kuongea na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vyama vya Ushirika, Baba Lishe na Mama Lishe, Maafisa Usafirishaji, wajane, wenye mahitaji maalum, Viongozi wa Serikali za mitaa, viongozi wastaafu pamoja na vikundi mbalimbali vya Ujasiliamali.

“Ndugu zangu wanalindi, CCM inatambua jasho lenu katika kujitafutia mali kupitia shughuli zenu mbalimbali kama kilimo, biashara na ujasiliamali, Serikali ya CCM itahakikisha inaweka mazigira wezeshi ili mnufaike na shughuli zenu zote” amesema Hamid

Aidha ameyaomba makundi mbalimbali ya kijamii, kuendelea kushirikiana na CCM kwa ukaribu zaidi kwa kukipa ushauri, mawazo na kutoa changamoto ili kupitia hayo Serikali ya CCM itazitafutia ufumbuzi.

Ameongezea kuwa, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kuacha tabasamu la kweli kwa kila mtanzania na kwa makundi yote ya kijamii.

Amesema, dhamira ya Rais ni kuona anaugwa mkono, ili kuleta maendeleo nchini, akisema kuwa ndio maana katika mapendekezo ya bajeti kuu ya Serikali 2026/2027 imekusudia kutenga asilimia 15 ya mapato ya halmashauri kutoa asilimia 10 ya awali ili kuongeza wigo katika upatikanaji wa mikopo.

Pamoja na hayo ameelekeza Serikali ya Mkoa wa Lindi na uongozi wa chama kutenga muda na kufanya mikutano maalum ya kuyasikiliza makundi ya kijamii.