January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

R4 za Samia zatawala maandamano ya CHADEMA yakikutana na msafara wa Dkt. Biteko Mbeya

Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraOline, Mbeya

DHANA ya R4 za Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kueleweka kwa wadau wa demokrasia nchini baada ya msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko kukutana na maandanano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku kila upande ukiendelea safari zake bila kubughudhi mwenzake.

Hayo yalijiri jana jijini Mbeya wakati wa msafara ya Dkt. Biteko ulipokutana na waandamanaji wa CHADEMA, lakini kila upande ulionekana kutekeleza kwa ueledi R4 za Rais Samia.

R4 hizo za Rais Samia ni maridhiano, ustahamilivu, mageuzi na kujenga upya sasa.

Kilichokidhihirisha jana kwenye maandamano hayo ni ustahamilivu, kwani waandamaji walisika wakifikisha ujumbe wao kwa Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Biteko kwamba wanataka Katiba Mpya.

“Mwimbie Naibu Waziri Mkuu kwa sauti kwamba tunataka katiba mpya…, Ndugu Waziri Mkuu kundi linalopita linataka Katiba Mpya, muimbie,” alisema mmoja wa washereheshaji wa maandamano hayo, huku waandamanaji wakiendelea kuiomba wanataka katiba mpya.

Mshereheshaji hiyo, aliwaambia kwamba upatikanaji wa Katiba mpya utasaidia kupugua kwa misafara mikubwa ya viongozi, kwani ni matumizi ya mabaya ya mali ya umma.

Kitendo cha kukutana kwa msafara ya Dkt. Biteko la maandamano ya CHADEMA, kinazidi kuipatia umaarufu Rais Samia, kwani miaka yote iliyopita, mikutano ya vyama vya siasa au maandamano yalizuiwa kufanyika pale ambapo kwenye mkoa fulani kama kulikuwa na ziara au shughuli za viongozi wa kitaifa au vyama vingine vya siasa.

“Kilichoonekana Mbeya leo (jana) ni kielelezo kwamba Rais Samia amefanikiwa kuijenga Tanzania yenye haki, demokrasia na usawa, ndiyo maana tulichokiona hakiwezi kuonekana nchi nyingi na hata hapa hakijawahi kutokea,” alisema John Mwambukile aliyekuwa kwenye maandamano hayo.

Amesema kitendo cha Rais Samia kuruhusu demokrasia itamalaki kwenye nchi yetu, kimewapunguzia hasira Watanzania na sasa hivi wanafikisha ujumbe wao kwa kwa watawala kwa misingi ya kuvumiliana.

Alisema mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia katika uwanja wa siasa na namna wadau walivyoelewa falsafa zake za 4R ni jambo la Pongeza.

“Sasa hivi nao wameanza kuelewa R4 maana hata Polisi wale waliokuwa kwenye msafara wa Dkt. Biteko hakuna aliyeshuka kwenye gari, lakini pia waandamanaji wa CHADEMA, waliachia upande mmoja msafara ukaendelea na safari, hii ni fundisho kwa nchi nyingine za Afrika,” Amesema Mbone Mwaikina.

Amesema miaka sita iliyopita kulikuwa na tofauti za kisiasa zilizosabbisha kutokuwa na majadiliano baina ya chama tawala na vya upinzani, lakini tangu Rais Samia aingie madarakani mazungumzo yanafanyika na leo (jana) wameona matokeo yake.

Amesema Rais Samia amefungua ukurasa mpya wa siasa. Maandamano ya CHADEMA yaliyoongozwa na viongozi wa CHADEMA yalihitimishwa kwenye Viwanja vya Luanda Nzovwe.

Miongoni mwa waandamanaji waliokuwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali. Maandano hayo yaliongozwa na Mwenyekiti Freemano Mbowe, na viongozi wengine wa juu yakimhusisha aliyekuwa Katibu Kuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa.