December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Queen Latifah kutunukiwa tuzo ya heshima BET Awards

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki na filamu toka nchini Marekani, Queen Latifah atatunukiwa tuzo ya heshima kwenye BET Awards 2021 (Lifetime Achievement Award), kutokana na mchango wake mkubwa kwenye muziki na kukuza utamaduni wa mtu mweusi.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Juni 27 mwaka huu katika ukumbi wa Microsoft Theater mjini Los Angeles, huku Mshereheshaji wa mwaka huu kwenye tuzo hizo ni Taraji P. Henson.

“Kwa zaidi ya miaka 20, Tuzo za BET zimekuwa sherehe ya ubunifu wa Weusi, sanaa na ubora,” amesema Henson, ambaye alicheza kwenye Dola la Fox na atatokea katika Annie Live ya NBC! mnamo Desemba.

“Onesho la mwaka huu litakuwa tofauti na kitu chochote kile ambacho tumewahi kuona hapo awali, na nimefurahi kushiriki jukwaa na wanawake wengi wenye nguvu na hodari katika muziki na burudani. Tuzo za BET zitakuwa mstari wa mbele katika utamaduni wa Weusi.” ameongeza.