Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
KAMPUNI ya kimataifa ya QNET inayojihusisha na bidhaa za mtindo wa maisha na ustawi kupitia mfumo wa mauzo ya moja kwa moja, imefanya mabadiliko katika muundo wa uongozi wake duniani na kikanda, huku Tanzania ikitajwa kuwa miongoni mwa masoko muhimu katika mkakati wake wa ukuaji barani Afrika.
Katika mabadiliko hayo, kampuni hiyo imemteua Jared Thwaits kuwa Meneja Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, akipewa jukumu la kusimamia shughuli na maendeleo ya kimkakati ya QNET katika nchi za kanda hiyo.
QNET imesema mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha huduma kwa wateja, kuongeza elimu kwa Wasambazaji Huru, kuboresha uzingatiaji wa kanuni na taratibu pamoja na kuongeza matumizi ya teknolojia katika shughuli za kampuni.
Kwa Tanzania, kampuni hiyo imesema uongozi wa kikanda utasaidia kufanya maamuzi kuwa karibu zaidi na wateja, Wasambazaji Huru na wadau wengine, ili kuiwezesha kampuni kuitikia kwa haraka mahitaji ya soko.
Thwaits pia atakuwa na jukumu la kuimarisha ushirikiano kati ya QNET na mamlaka za udhibiti, vyombo vya habari, makundi ya watumiaji pamoja na wadau wengine.
Hatua hiyo inalenga kuongeza uelewa kuhusu biashara halali ya mauzo ya moja kwa moja na kukabiliana na taarifa potofu zinazohusishwa na sekta hiyo.
Uteuzi wa Thwaits ni sehemu ya mabadiliko mapana ya uongozi wa QNET duniani, huku timu mpya ya uongozi ikijumuisha Mattias Mildenborn ambaye ameteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), Elena Khoo kuwa Afisa Mkuu wa Masoko (CMO), Peter Luk kuwa Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) na Ben Bredenkamp kuwa Afisa Mkuu wa Habari wa Kundi (Group CIO).
Mkurugenzi Mkuu wa Kundi la QI Group, kampuni mama ya QNET, Kuna Senathirajah, amesema mabadiliko hayo yanalenga kuunganisha viongozi wenye uzoefu ili kuendeleza ubunifu, kuboresha huduma kwa wateja na kuiandaa kampuni kukidhi mahitaji ya kizazi kipya.
Amesema QNET inalenga kuwapatia Wasambazaji Huru maarifa, teknolojia na msaada unaohitajika ili kujenga biashara endelevu na zenye uwajibikaji.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, Afrika ni eneo muhimu katika mkakati wake wa muda mrefu, huku Tanzania ikitajwa kuwa na fursa kutokana na idadi kubwa ya vijana, matumizi ya teknolojia na utamaduni wa ujasiriamali.
Chini ya uongozi wa Thwaits, QNET imeeleza kuwa inalenga kuimarisha ushirikiano na wateja, Wasambazaji Huru na wadau nchini Tanzania, sambamba na kuongeza uwekezaji katika elimu, teknolojia na uzingatiaji wa kanuni.
Akizungumzia soko la Tanzania, Thwaits amesema nchi hiyo ni muhimu kwa QNET na ina fursa kubwa ya muda mrefu.
“Tanzania ni soko muhimu kwa QNET na tunaona ina fursa kubwa ya muda mrefu. Hata hivyo, ukuaji endelevu hauhusu kupanua biashara pekee, bali pia kuhakikisha kuwa wateja wanaelewa bidhaa zetu, Wasambazaji Huru wanatambua wajibu wao na wadau wanapata taarifa sahihi kuhusu mfumo wetu wa biashara,” amesema.

More Stories
Tuzo za Wafugaji kuongeza tija ya Mifugo
Kigoma yatoa tenda zaidi ya Milioni 500
TMDA yakamata dawa zisizosajiliwa JNIA