Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira Mazuri ya uwekezaji ambayo yamesababisha kuweza kukabidhi gawio la Shilingi Bilioni 12.2 kwa Serikali na kuahidi kuendelea kuboresha huduma zao ili kufanya vizuri zaidi.
Gawio hilo wamelikabidhi leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt. Samia na kumepokea gawio kutoka kwa Kampuni 10 ambazo Serikali inahisa zake na Kampuni hiyo ni miongoni mwa Kampuni hizo.
Akizungumza baada ya kukabidhi gawio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Abdallah amesema wanamshukuru Rais Dkt. Samia ambaye ndio jemedari wetu wa kiuchumi nchini.
“Ameweza kutuongoza vizuri, ameweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kufanya biashara kwa usalama na ubunifu,Pia tunatoa shukrani kwa Wizara ya Nishati chini Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko wamekuwa ni viongozi ambao wakituelekeza na kutushauri lakini wamekuwa wakiweka mazingira yanayotuwezesha kufanya kazi vizuri.
“Pia tunamshukuru Msajili wa Hazina ambaye amekuwa kiungo muhimu kwetu sisi kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri na hatimaye tumetoa gawio la bilioni 12.2, Kigezo kikubwa ambacho kimewazesha kutoa gawio hilo kinatokana na kufanya kazi vizuri kwa Bodi yetu chini ya Mwenyekiti Dkt. Selemani Majige ambao wamekuwa wakituelekeza na kutupa ushauri mzuri,” amesema Fatma Abdallah.
Akieleza zaidi katika kuendeleza ufanisi wa kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma na kuziboresha na kwamba mikakati yao ni kutoa huduma kidigitali katika kuwafikia watanzania wengi kwenye kusambaza nishati.
Pia amesema wameona Serikali ilivyoweka nguvu katika nishati safi hivyo na wao wameamua kuweka nguvu katika kufanikisha malengo ya Serikali katika eneo la Nishati Safi ya kupikia kama ilivyo dhamira ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi.
Pia amesema Wanampango wa kuzindua kituo cha gesi kwa ajilli ya kujaza katika magari na uzinduzi huo wanatarajia kuufanya mwaka huu huku akisisitiza wanajivunia kutoa gawio hilo kwani kumekuwa na ongezeko kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa