*Mshindi wa droo ya vilainishi apata Elite Card ya shilingi milioni 5.
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
Kampuni ya Puma Energy imeendelea uelimisha watumiaji kuhusu umuhimu wa kutumia vilainishi halisi vinavyotolewa na vituo rasmi vya mafuta pamoja na kuwekeza katika kupanua upatikanaji wa huduma zake .
Hatua hiyo inalenga kuepuka athari za bidhaa bandia zinazoongezeka sokoni na kuhakikisha wateja wanapata bidhaa salama na zenye ubora.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Oil Puma Energy, Matiko Bugumia,baada ya kumtangaza na kumkabidhi mshindi wa droo ya vilainishi, Boaz Aywayo.
Mshindi huyo alipatiwa zawadi ya kadi ya Elite(Elite Card) yenye thamani ya shilingi milioni 5, ambayo itamuwezesha kufanya manunuzi ya vilainishi au gesi katika kituo chochote cha Puma nchi nzima.
Droo hiyo pia iliwazawadia washindi wengine vilainishi na fedha taslimu kama sehemu ya kampeni ya kuwashukuru wateja wa Puma Energy.
Bugumia amesema droo hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni kuongeza thamani kwa wateja wake na kuendelea kuhimiza matumizi ya vilainishi halisi.
“Soko limekua kwa kasi, lakini changamoto ya bidhaa bandia bado ipo. Ndiyo maana Puma Energy inaendelea kutoa bidhaa bora na salama ili kulinda magari na vifaa vya wateja wetu,”amesema Matiko.
Kwa upande wake, mshindi wa droo, Boaz Aywayo, ametoa rai kwa wateja wengine kununua bidhaa kwenye vituo vinavyoaminika.
“Bidhaa bandia ni changamoto, lakini Puma Energy imethibitisha kuwa chanzo cha bidhaa salama na zilizothibitishwa,” amesema Boaz.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako