Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
PUMA Energy Tanzania imetunukiwa tuzo mbili ambazo ni kampuni inayopendwa zaidi ya mafuta na nishati Barani Afrika na kituo cha mafuta kinachotoa huduma kwa wepesi na kupatikana kwa urahisi.
Katika hafla ya Consumer Choice Awards, imeelezwa kuwa tuzo hizo zilizopigiwa kura na watumiaji pamoja na wataalamu wa sekta ni uthibitisho wa mkakati wa kampuni katika kutoa bidhaa bora za mafuta na nishati, mtandao mpana wa vituo vya kisasa, na kiwango cha juu cha utoaji wa huduma.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah amesema tuzo ya kampuni inayopendwa zaidi ya mafuta na nishati Barani Afrika ni uthibitisho wa taswira chanya ya kampuni hiyo barani kote.
Pia ni picha ya uaminifu, weledi wa kiutendaji na suluhu bunifu za nishati pamoja na kuonesha imani ambayo mamilioni ya watumiaji, wafanyabiashara na washirika wanaendelea kuwa nayo kwa PUMA Energy katika shughuli zao za kila siku.
Wakati huo huo, tuzo ya kituo cha mafuta kinachotoa huduma kwa wepesi na kupatikana kwa urahisi inaonesha ubora wa utekelezaji wa kampuni chini hapa.
Pia amesema kampuni hiyo imewekeza kwa uthabiti kwenye maeneo ya kimkakati, miundombinu ya kisasa na huduma zinazokidhi mahitaji ya madereva wa kisasa wa Kitanzania kuanzia vituo vyenye mwanga wa kutosha, usalama, usafi wa mazingira, malipo ya kidigitali, hadi mtandao mpana unaohakikisha kituo cha PUMA hakiko mbali na mteja.
Kwa upande wake Mkuu wa Sheria na Masuala ya Ushirika wa Puma Energy Tanzania, Emmanuel Bakilana, amesema,wanajitahidi kila mara kuhakikisha mteja yupo katikati ya kila wanachofanya.



More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi