January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PST yapokea mikanda ya ubingwa

Na Yusuph Digossi, TimesMajira Online

SHIRIKISHO la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) tayari limeshapokeo mikanda yote ya ubingwa kuelekea kwenye mashindano ya ‘Open Air International Boxing’ yatakayofanyika Oktoba 16, 2020.

Mapambano hayo ya wazi yatafanyika katika Uwanja wa Mabembeauliopo Keko Magusumbasi na hayatakuwa na kiingilo.

Katika mapambano hayo, bondia Mtanzania Innocent Evarist atapanda ulingoni kuzichapa na bondia kutoka Uingereza Prince Patel kuwania ubingwa wa ‘WBO Global & Africa’ katika pambano la raundi 12 uzito wa kilogramu 52.16 Super Flyweight.

Mabondia kutoka Tanzania Julias Kisarawe na Salum Msabaha watawania ubingwa wa UBO All Africa and PST
katika pambano la raundi 10 uzito wa kilogramu 52.16 Super Flyweight

Kwa upande wake, Mtanzania Issa Mbwana atamkaribisha Muingereza, John Brennan katika pambano lisilo la ubingwa la raundi nane uzito wa kilogramu 69.85 Super Welterweight huku watanzania Singa Chala na Yusuph Shamsani wakipigana raundi nne.

Lakini pia kutakuwepo na pambano la wanawake ambapo bondia wa Tanzania Halima Vinjabei atamkaribisha bondia kutoka nchini India katika pambano la raundi 10 uzito wa kilogramu 48.98.