NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO.
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na kutoa elimu kwa
wanachama na wananchi wanaotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Siku
ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, viwanja vya Tumbaku mjini
Morogoro, pia unapita “Banda kwa Banda”
ili kuwafikia wanachama wake, Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi
amesema.
Bw.
Njaidi amesema Mfuko unashiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu na
kuwahudumia wanachama wake ambao ni wastaafu lakini pia watumishi wa Umma na
Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa asilimia 30.
“Lakini
tukumbuke kuwa watumishi walio kwenye viwanja hivi nao pia wanawahudumia
wananchi kwenye mabanda yao, hivyo tumeona tugawane majukumu, baadhi yetu wako
bandani kutoa elimu na huduma kwa watakaofika na sisi tunapita banda kwa banda
kuwahudumia.” Alifafanua Bw. Njaidi ambaye alifuatana na Afisa Matekelezo Mwadamizi wa Mfuko huo Bw. Charles Mahanga.
Akifafanua
alisema kwakuwa huduma nyingi za Mfuko zinapatikana kiganjani (PSSSF Kiganjani)
hivyo ni rahisi kuwapatia elimu kwenye mabanda yao ya jinsi ya kutumia huduma
hiyo.
Kilele
cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi
hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine
duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha
uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi
ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni
kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”.
Banda la OSHA
More Stories
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang