NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unaingiza karibu bilioni 200 kila
mwezi kwenye uchumi wa nchi kupitia malipo ya Mafao wanayolipa Wanachama wake,
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo, Bw. James Mlowe amesema.
Bw.
Mlowe ameyasema hayo kwa nyakati tofauti kwenye ziara yake ya kutembelea vyombo
vya habari jijini Dar es Salaam iliyokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akifafanua
Bw. Mlowe amesema, PSSSF ina wastaafu 150,000 ambao hulipwa shilingi bilioni 60 kama
malipo ya pensheni ya kila mwezi sambamba na kulipa zaidi ya shilingi bilioni
120 kila mwezi kama malipo ya Mafao mbalimbali kwa wanachama ambao bado
hawajafikia umri wa kustaafu.
“Wastaafu
na wanachama wetu wamesambaa kila kona ya nchi, wastaafu wengi pensheni yao
siyo pesa ya kuwekeza ni ya matumizi ambayo inaenda kwa mama ntilie, na huduma
mbalimbali za kijamii kwa hivyo inachachua uchumi, kwa hiyo bilioni 120
ukijumlisha na bilioni 60 ni bilioni 180 na wakati mwinhine hufikia shilingi
bilioni 200 ambazo kila mwezi zinaenda kwenye uchumi wa nchi.” Alifafanua Bw.
Mlowe.
HUDUMA
ZA TEHAMA
Akizungumzia
maboresho ya utoaji huduma kwa Wastaafu na Wanachama wa Mfuko huo Bw. Mlowe
ambaye alifuatana na Afisa Uhusiano Mkuu Bw. Abdul Njaidi alisema, Mfuko
umeimarisha mifumo yake ya TEHAMA ambapo Mwnachama na Mwajiri wanawasiliana na
Mfuko kwa urahisi zaidi kwa njia ya kidijitali.
“Tuna
huduma za PSSSF Kiganjani na huduma ya PSSSF Popote Ulipo Mtandaoni, lakini pia
Wastaafu ambao wanatakiwa kujihakiki kila mwezi sasa wanajihakiki kupitia alama
za vidole (Biometric).” Alifafanua.
MALIPO
YA MALIMBIKIZO YA PENSHENI YA KILA MWEZI
Bw.
Mlowe amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kuuwezesha Mfuko kulipa Malimbikizo ya Pensheni ambapo ametoa cash
bond ya shilingi trilioni 2.17 sawa na asilinmia 50% ya deni na tayari ameanza
kuweka pesa hizo.
“Ni
uamuzi wa kupongezwa ameufanya Mhe. Rais, kwani tayari tumelipa malimbikizo
yanayofikia shilingi trilioni 1 na sasa tunaendelea na kulipa mafao mapya ya
hivi sasa.” Alifafanua.
UWEKEZAJI.
Alisema
Mfuko unawekeza kwa kufuata Sera ya Uwekezaji ya Mfuko, miongozo/kanuni za
Benki Kuu ya Tanzania na Wizara yenye dhamana ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
“Tumewekeza
kwenye Ardhi na Majengo, Dhamana za Serikali (Government Bonds), Amana za
Mabenki, Hisa kwenye soko la Mitaji na Viwanda.”
Akifafanua kwanini Mfuko unawekeza, Bw. Mlowe alisema “Kulinda thamani ya michango ya wanachama, kuboresha mafao kwa wanachama na kuchangia juhudiza serikali kuinua uchumi wan chi.”
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. James Mlowe (kulia) akiwa na Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi akifafanua jambo wakati alipotembelea chumba cha habari cha magazeti ya Chama Uhuru barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam.
More Stories
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao