November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Profile yaendeleza ubabe MRBA

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Mwanza

BINGWA mtetezi wa mashindano ya mpira wa kikapu ya Ligi ya Mkoa wa Mwanza (MRBA), timu ya Profile imeendeleza ubabe baada ya kuwafunga Octopus kwa pointi 80-72.

Hadi sasa katika mashindano hayo timu hiyo imeshacheza mechi mbili lakini ikiendelea kulinda rekodi yake ya kutopoteza mechi.

Mcheziji wa mabingwa hao watetezi Shaban Ally ‘Bobo’ alifanikiw akufunga pointi 33 na Daniel Malaki wa Octopus alifanikiwa kufunga pointi 18 .

Kwa Shaban Ally kufanikiwa kufunga pointi hizo ni mwendelezo mzuri kwa kile anachokifanya katika mashindano hayo baada ya kufanikiwa kufunga pointi 29 katika mchezo wao uliopita dhidi ya Dolphin.

Katika mechi nyingine zilizochezwa kwenye mashindano hayo, timu ya SAUTI imefanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi 79 dhidi ya 72 za Orotalio.

Kamishna wa Mashindano na Ufundi wa MRBA, Haidari Abdul ameuambia Mtandao huu kuwa, matokeo hayo yanadhihirisha kuwa Profile imeendelea kufanya vizuri baada ya kutopoteza mchezo kati ya miwili waliyocheza hadi sasa.

Amesema, hadi sasa Ligi inaendelea vizuri na vipaji vipya vimeanza kuonekana pamoja na kuwa mechi zimeanza kuwa ngumu kwa kila mmoja.

“Tumeona mechi kati ya Orotalio na Sauti matokeo yalikuwa ni yale ya kubanana na mtu yoyote alikuwa na uwezo wa kupoteza hivyo tunawaomba mashabiki pamoja na wapenzi wa mchezo huu wafike kwa wingi ili kuwapa sapoti wachezaji, ” amesema Kamishna huyo.

Hata hivyo mbali na Profile ambao wameshinda mechi zote mbili, timu ya Octopus yanyewe imeshinda mechi mbili na kupoteza moja, Dolphin imeshinda mechi moja, SAUT imeshinda mechi moja, Cuhas imeshinda mechi mbili na kupoteza mbili, Orotalio ikishinda mechi moja na kupoteza mechi moja wakati Eagles ikishinda mechi moja na kupoteza moja.

Hata hivyo kuongozi huyo alisema kuwa, baada ya michezo hiyo, wishoni mwa wiki kutakuwa na mechi nyingine huku mechi hizo zikiendelea hadi Septemba ambapo watapata timu mbili kwa ajili ya kushiriki mashindano ya NBL.