Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma
KATIBU Mkuu Wizara ya Maji, Professa Kitila Mkumbo ameonyesha kukerwa na lugha chafu zinazotolewa na baadhi ya watumishi katika mamlaka za maji nchini.
Kufuatia hali hiyo, Mkumbo amewaonya watumishi wenye tabia hizo huku akizitaka kuwahudumia wateja inavyostahili badala ya kuwajibu wateja majibu yasiyofaa.
Pia amezitaka mamlaka hizo kuwa wabunifu katika utendaji kazi kwa maendeleo ya sekta hiyo na taifa kwa ujumla.
Profesa Kitila amesema hayo jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya utendaji kazi baina ya Wizara ya Maji na Bodi za Maji na Mabonde na Mamlaka za Maji Safi na Mazingira.
“Baadhi ya Mamlaka za Maji zimekuwa na majibu yasiyofaa kwa wateja wa maji, zipo lugha ambazo wanapewa wateja zinatisha, hali hii haikubaliki hata kidogo” amesema Profesa Kitila na kuongeza
Awali akitoa taarifa za mikataba ya utendaji wa bodi za maji ya mabonde kwa mwaka 2019/2020, Mkurungezi Idara ya Rasilimali za Maji Dkt Genge Lugomela amesema kuwa kila bodi ya maji ya bonde inatakiwa kutumia asilimia 30 ya mapato yake.
Kwa upande wake Mkurungezi Idara ya Usambazaji Maji, Mhandisi Nadhifu Kemikimba amesema zoezi hilo linahusisha mamlaka za maji 69 na katika mamlaka hizo mamlaka za miji mikuu ya mikoa ni 26 na mamlaka za miradi ya kitaifa zilikuwa nane lakini sasa zimebaki saba baada ya Chaliwasa kuunganishwa na Dawasa.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini