December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof. Ndalichako azitaka Taasisi za Umma, binafsi kuwasilisha michango ya watumishi wao

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Imeelezwa kuwa sababu ya wastaafu wengi kusota kwa zaidi ya miaka minne bila kupata mafao yao ni kutokana na Halmashauri mbalimbali nchini kushindwa kuwasilisha michango ya watumishi wao kwa wakati.

Hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amezitaka taasisi za umma na binafsi kuwasilisha michango ya watumishi wao kwa kuwa hilo ni takwa la kisheria.

Profesa Ndalichako,ametoa maagizo hayo wakati, akizungumza na wastaafu jijini Mwanza kutoka Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani ambapo ameeleza kuwa chanzo cha waliokuwa watumishi hao kuchelewa kupata mafao yao ni kutokana na waajiri kushindwa kuwasilisha michango yao kwenye mifuko ya jamii

“Nazitaka hizi taasisi zikiwemo za Uma na binafsi zinazopeleka mifuko ya hifadhi ya Jamii NSSF na PSSSF kuhakikisha zinawasilisha michango ya watumishi wake kwa wakati ili kuwasaidia wanapostaafu waweze kulipwa mafao yao,”ameeleza Profesa Ndalichako.

Hata hivyo baadhi ya wastaafu waliofika katika kikao hicho wamemshukuru waziri Ndalichako kwa kutenga muda na kuwasikiliza kwani imeleta matumaini makubwa ya matatizo waliyokuwa wanapitia.

Mmoja wa wastaafu hao Haido Ngowi ameeleza kuwa baada ya kusikilizwa anaamini kuwa waliopewa dhamana na Waziri kushughulikia matatizo yao watayafanyia kazi kwa uharaka zaidi.

Baadhi ya wastaafu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako(hayupo pichani) katika kikao cha Waziri huyo na wastaafubhao cha kusikiliza malalamiko yao kilichofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako,akimsikiliza mmoja wa wastaafu waliohudhuria kikao maalumu cha Waziri huyo cha kusikiliza changamoto zao na malalamiko yao kilichofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)