December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof Ndalichako akutana na wastaafu zaidi ya 1000 Dar, atoa wito kwa mashirika 

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako katika muendelezo wa kukutana na wastaafu nchi kwa lengo la kutatua Changamoto zao mbalimbali, Zaidi ya Wastaafu 1000 wa Dar es salaam wanaohudumiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, NSSF na PSSSF wamejitokeza katika Mkutano huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Waziri Ndalichako leo Julai 22, 2022  katika ofisi za NSSF amesema  kazi imeanza ya kuwasikiliza Wastaafu na kutatua Changamoto  na  wizara yake pamoja na Mambo mengine ina dhamana ya kusimamia Wastaafu wanaolipwa mafao Kupitia Mfuko wa NSSF na PSSSF.

Amesema anatambua kuwa wapo wastaafu ambao wanalipwa mafao yao kupitia Hazina kuwa wakifika katika mkutano huo kuna fomu watapewa kwa ajili ya kuzijaza na baadaye fomu hizo zitawasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango.

“Tunao uwezo wa kutatua changamoto moja kwa moja za wastaafu ambao wanalipwa kupitia Mfuko wa NSSF na PSSSF,”amesema Waziri

Waziri Ndalichako amesema anathamini mchango mkubwa uliotolewa na wazee katika ujenzi wa Taifa hivyo atahakikisha kwa kushirikiana na watendaji wa NSSF na PSSSF changamoto zao zinasikilizwa, kutatuliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Aidha Amesema miongoni mwa changamoto za wastaafu aliokutana nao ni pamoja na mapunjo ya mafao na huku akisisitiza kuwa changamoto zote zitapatiwa ufumbuzi na kila mstaafu atapata huduma anayostahiki.

Kwa upande wa mstaafu kutoka Hospital ya Muhimbili Jane Mahige,  amesema wanamshukuru Rais Samia Suluh Hassani kwa kumuagiza Waziri Ndalichako kuja kuongea na waastafu.

“Wastaafu tulikuwa na madukuduku Mengi ,mafao yanacheleshwa lakina Leo tumekuja NSSF na tume elimishwa kwa ambayo tuliokuwa hatuelewi tumeelewa na tunalipwa kutokana na kiwango Cha mishara yetu na watumishi wa NSSF wametupokea vizuri” amesema Jane.

ReplyForward