January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza

Fresha Kinasa, TimesMajira Online, Mara.

MBUNGE  wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara  Prof.  Sospeter Muhongo, ametoa pongezi nyingi kwa vijana 32, wa Musoma Vijijini  waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza, tarehe 9 -13 Octoba 2024 ,ili kushiriki Nyerere Day ambapo amesema  kuwa kitendo hicho  ni alama  ya  uzalendo mkubwa waliouonesha. 

Amesema jambo hilo,lilifanywa na Hayati  Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa azimio la Arusha mwaka 1967.

Prof. Muhongo ameyasema hayo Disemba  21, 2024 wakati wa kikao Cha Baraza la Vijana wa CCM  (UVCCM) Wilaya ya Musoma Vijijini alipokuwa mgeni rasmi kwenye Baraza hilo  ambapo kikao hicho  kilifanyika Kijijini Murangi makao makuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya hiyo.

Tarehe 14 Octoba 2024, vijana hao walishiriki kwenye sherehe za uzimaji wa Mwenge wa Uhuru (Nyerere Day), Jijini Mwanza. Na Mbunge huyo alitoa michango ya kusaidia ushiriki wao na vijana wengine wote kwenye matembezi hayo akawahimiza kuwa wazalendo, waadilifu,kulinda amani  na kutumika kwa maslahi mapana ya Taifa.

“Vijana imara na shujaa
wote 32 wa Musoma Vijijini walifika Mwanza bila tatizo lolote,pongezi nyingi kwao”amesema Prof. Muhongo.

Aidha, Mbunge huyo ametoa ushauri kwa Vijana hao 32 na kuwahimiza  waanzishe miradi ya kiuchumi Maeneo yenye fursa za kujiajiri na kukuza uchumi wao. Ambapo  yameainishwa kwenye Kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya ya Musoma Vijijini.

Aidha vijana hao wamemshukuru Prof. Muhongo kwa kuendelea kushirikiana nao kwa karibu na kuwapa mbinu, ushauri na maarifa mbalimbali yatakayowatoa kimaisha.