January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Muhongo atunukiwa tuzo ya pongezi  Musoma Vijijini

Fresha Kinasa, TimesMajira Online, Mara.

BARAZA la Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi la Wilaya ya Musoma Vijijini limemtunuku Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof.Sospeter Muhongo, Tuzo  ya pongezi  kwa kutambua ushiriki wake na mchango wake mkubwa wa fedha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika tarehe 27.11.2024.

Prof.Muhongo amekabidhiwa tuzo hiyo katika Kikao cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Musoma Vijijini kilichofanyika Kijijini Murangi  Dicemba 17, 2024. Ambapo mgeni rasmi alikuwa  Simon Rubugu ambaye ni Katibu wa Siasa, Mwenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Mara.

Ushiriki wa Prof.Muhongo kwenye Uchaguzi umetajwa kuwa ni pamoja na Kuelezea wananchi (wapiga kura) mafanikio makubwa ya Serikali  inayoongozwa vizuri na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Na
Pia Kuelezea wananchi mafanikio makubwa yanayopatikana Jimboni humo kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

Pia, Kuelezea wananchi jimboni humo  vipaumbele vya sasa na vya miaka ijayo vya mahitaji ya wananchi wa Jimbo la hilo na Kutoa michango mikubwa ya fedha kugharimia uchapishaji na ugawaji wa vitabu viwili vya rangi  vinavyoelezea miradi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
jimboni humo nakala 1,500.

Ushiriki mwingine wa Prof. Muhongo ni utoaji wa Posho za mawakala wakati wa upigaji kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) matawi 95, usafiri kwenye kampeni za wagombea wa CCM nafasi za Serikali za Vijiji 68,usafiri wa wapiga kampeni wakiwemo viongozi watatu kutoka kila Kata jumla ya  Kata 21.”

Aidha utoaji wa magari manne (4) yaliyotumiwa kwenye kampeni,
usafiri wa boti (mafuta & posho) kwenda kwenye kampeni za visiwa vitatu (3) vikubwa na posho za washiriki mbalimbali wa kampeni.

“Pia Viongozi wa Chama (CCM) na Jumuiya zake Wazazi, UWT na UVCCM) ngazi za Wilaya, Kata, Matawi walishiriki kwa kujituma ipasavyo hadi kupata ushindi mkubwa kwenye Uchaguzi huo. Ambapo  Vijiji ni  68 na CCM 66 (97.06%), CHADEMA Vijiji 2, Vitongoji ni  374  ushindi CCM 358,   (95.72%) na  CHADEMA 16.”imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge.

Kwa upande wao Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini akiwemo Fabian Mafuru Mkazi wa Kata ya Bukumi amesema Prof. Muhongo ameendelea kushiriki kikamilifu katika agenda ya maendeleo jimboni humo. Na pia   kuwaunganisha pamoja  Wananchi kushirikiana na Serikali kuchangia maendeleo.