Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza
Licha ya kuwepo kwa ongezeko la unywaji maziwa kutoka wastani wa lita 20 mwaka 1997 hadi lita 67.5 mpaka kufikia sasa kwa mtu mmoja kwa mwaka imeelezwa kuwa sekta ya maziwa nchini inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinachangia kukwamisha maendeleo ya sekta hiyo.
Ambapo miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na suala zima la ufugaji,“ufugaji wetu ni ule wa kuhamahama siyo wa kisasa,moja ya malengo ya maadhimisho haya ni kuwaelekeza watanzania kwenda kwenye ufugaji wa kibiashara,wa kisasa na wa ng’ombe bora ambao watatupatia maziwa mengi nchini kuliko ng’ombe wengi tulionao na kusifika kuwa Tanzania ni wa pili Afrika kwa wingi wa mifugo huku tukiwa na ng’ombe ambao wanatupatia maziwa kidogo sana huku wakiharibu mazingira,”ameeleza Profesa George Msalya.
Hayo yamebainishwa Mei 29,2024 na Msajili wa Bodi ya Maziwa,Profesa George Msalya wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 27 ya wiki ya maziwa kitaifa yanayofanyika kitaifa mkoani Mwanza katika uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela mkoani hapa yenye kauli mbiu “Kunywa maziwa salama kwa afya bora na uchumi endelevu yalioanza Mei 28 hadi Juni Mosi mwaka huu.
Sanjari na hayo Profesa Msalya amefafanua kuwa mnyororo wa thamani wa maziwa unaanzia kwa wadau wanaowapa rasilimali mbalimbali ikiwemo vyakula vya mifugo,dawa za mifugo,watoa hudama za afya,malisho,mbegu za malisho na mifugo yenye pia wazalishaji na wasafirishaji.
“Tuna watu mbalimbali mpaka wanapokwenda kwa mlaji lakini hapa katikati wapo watunga sera,vyombo mbalimbali ambavyo vinasimami sheria,mazingira,ukitaka kujua changamoto tulizonazo lazima utazame mnyororo wa thamani tukiangalia wale watu wanaotupa rasilimali mbalimbali bado tuna ufeki katika dawa za mifugo,pia hazitunzwi vizuri,hivyo katika kuchoma wale ng’ombe na kuwahudumia wakati mwingine tunapata jambo la uchanganyaji wa dawa na maziwa kwa sababu ng’ombe anapopewa dawa wakati mwingine dawa inaingia katika maziwa,”
Pia ameeleza kuwa kwenye usafirishaji bado hawajapata miundombinu ya kutosha hivyo wanahitaji vituo 700 vya kukusanyia maziwa nchi nzima vilivyopo ni vituo 252,wakusanyaji ni wachache huku yakisafirishwa kwa njia ya mabasi kitu ambacho siyo sahihi kwani tunaweza kuyaharibu.
Aidha ameseka changamoto nyingine ni suala la ulaji bado,kwenye huduma za ugani pia kwani Maofisa Ugani hawatoshi waliopo ni 3,800 na wanahitaji 17,000 nchi nzima,gharama za usindikaji na vifungashio zipo juu kwani vipo viwanda vichache vya vifungashio na siyo imara vingi wanavipata kutoka nje ya nchi.
Pia matenki ya kuhifadhia maziwa yanapatikana nje ya nchi kwa gharama kubwa ambapo tenki moja la lita 200 linauzwa kwa shilingi milioni 15 na kuendelea huku serikali ikiendelea kushughulikia changamoto hizo kwa kufuta kodi kwa baadhi ya vifaa vya kuhifadhia,kusafirishia na kubebea maziwa.
“Tunaendelea kuona ‘impact’matokeo na tuanaendelea na mipango ya kukabiliana na changamoto hizo lakini kazi inafanyika,tulipo anza maadhimisho kwa mara ya kwanza mwaka 1997 tulikuwa tunakunywa maziwa lita 20 leo tunakunywa lita 67.5 kwa mtu mmoja kwa mwaka,uzalishaji miaka kadhaa tulikuwa lita bilioni 2,lakini leo tunazungumza lita karibu bilioni 4 kwaio licha ya changamoto tunazokutana nazo kazi inafanyika na jitihada kubwa zinafanywa na serikali za kuhakikisha kwamba tunafikia nchi ya ahadi,”.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba