June 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Mkenda:Wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Mtihani walifanya wizi katika mitihani

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknlojia Profesa Adolf Mkenda ametolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya wazazi wa watoto waliofungiwa matokeo ya mitihani ya kidato nne mkoani Mwanza huku akisema ,matokeo ya watoto hao yamefungiwa kutokana na wizi wa mitihani uliojionyesha dhahiri.

Profesa Mkenda amekanusha malalamiko yaliyodai kwamba watoto wa vigogo pekee ndiyo ambao hawakufutiwa mitihani huku akisema watoto wote ambao majibu yao yakuwa ya kunana ,hawajafutiwa wala kufungiwa matokeo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma Profesa Mkenda amesema,kupitia Baraza la Mitihani la Taifa,Wizara yake imepitia kila kundi la wale ambao matokeo yao yamefutwa na kujiridhisha kwamba watoto wote waliofutiwa mitihani ya kidato cha nne mwaka jana wamehusika kwenye ubadhirifu huo .

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne walikuwa 560,335 kati ya hao wanafunzi ambao wamefutiwa matokeo ni 337  sawa na  asilimia 0.06 ya watahiniwa wote.

Akiainisha makundi ya watahiniwa hao waliofanya udanganyifu katika mitihani hiyo ya kidato cha nne mwaka jana ,Profesa Mkenda amesema, wanafunzi 20 matokeo yao yamezuiwa kwa sababu uchunguzi bado unaendelea na utakapokamilika NECTA  litachukua hatua stahiki kulingana na matokeo ya uchunguzi yatakayopatikana .

Vile vile amesema,katika wanafunzi waliofutiwa matokeo wapo wanafunzi wanne ambao waliandika matusi kwenye vitabu vyao vya kuandika majibu na matokeo yao yamefutwa kulingana na kanuni zinazoongoza uendeshaji wa mitihani  lakini pia wapo wanafunzi 51 waliokutwa kwenye vyumba vya mitihani wakiwa na maandishi yasiyoruhusiwa kwenye vyumba vya mitihani huku wengine wakikutwa na  vitabu au booklet na matokeo yao yalifutwa .

“Wapo wanafunzi kumi waliokamatwa na ama simu ama ‘smart watch’ kwenye vyumba vya mitihani wakati wanafunzi wote wanajua kwamba hawaruhusiwi kuingia na vitu hivyo kulingana na kanuni za uendeshaji wa mitihani,

“Wapo watahiniwa tisa wenyewe hawakwenda kwenye vyumba vya mitihani walituma watu wengine wakawafanyie mitihani na walikamatwa na wasimamizi ,na picha za watahiniwa wote zipo na hao tisa wote walioenda kuwafanyia watu wengine mitihani walikamatwa na polisi lakini waliotakiwa wafanye mitihani matokeo yao yamefutwa.”amesema Profesa Mkenda na kuongeza kuwa

“Wapo wanafunzi 27 walikamatwa wakisaidiana kwenye chumba cha mtihani kinyume na kanuni za mitihani na wenyenwe matokeo yao yamefutwa…,wapo watahainiwa sita matokeo yao yamefutwa kwa sababu ya kutumia jukwaa la whatsapp kusaidiana.”

Amesema hilo lilitokea  kwenye shule inaitwa Mnemonic Academy ya Mjini Magharibi Zanzibar ambapo mtahiniwa mmoja aliingia na simu ambapo alipiga picha ya mtihani na kuituma kwa mwenye shule ambaye alitengeneza majibu ambayo aliyarusha  kwenye group la whatsapp.

“Katika watahiniwa waliokuwa wanafanya mtihani ukimwacha huyu mmoja ambaye alikutwa na simu ,wapo wengine watano waliokuwa kwenye group hilo ingawa hawakukamatwa na simu lakini walikuwa kwenye group hilo, matokeo yao yamefutwa kwa sababu walionyesha jitihada za kudanganya,unaweza ukawekewa majibu kwenye simu yako ukatoka kwenda kujisaidia ukaangalia majibu ukarudi tena kufanya mtihani.”amesema na kuongeza kuwa  

“Lakini wapo watahiniwa wengine 20 matokeo yao yamezuiwa hayajafutwa kwa sababu katika lile group la whatsapp ambayo majibu yalirushwa tuna majina 20 ambayo hayalingani na waliofanya mitihani hayafahamiki ni wakina nani kwa hiyo uchunguzi unaendelea kuhakiki kabisa waliokuwa na zile namba za simu ni akina nani na matokeo yake yatakayopatikana ,na Baraza  litachukua hatua stahiki ,lakini kesi hii ipo polisi kwa ajili ya uchunguzi.”

Hata hivyo Profesa Mkenda amesema Academy hiyo imefutwa kama kituo cha mitihani nani kati ya zile shule ambazo huenda zikafutiwa usajili wake moja kwa moja.

Katika hatua nyingine amesema,wapo wanafunzi 206 wamefutiwa matokeo kwa sababu ya kufanana kusiko kwa kawaida kwa majibu waliyotoa kwenye mitihani yao, kati yao wanafunzi 140 wanatoka katika shule/kituo cha Thaqaafa  cha jijini Mwanza ambacho ndiyo wazazi waliandamana, na watahiniwa 66 wanatoka katika kituo cha mitihani au shule inaitwa Twibhoki ya mkoani Mara.

“Kilichotokea wakati mtihani unafanyika taarifa za siri ziliwasilishwa kwenye baraza kwamba, kuna wizi na udanganyifu mkubwa unaendelea wa mtihani,Baraza  likachukua hatua mbalimbali lakini wakati wa kusahihisha ,baraza la mitihani liliamua kupitia majibu ambayo yalitolewa na ukipitia majibu hayo ,utaona maswali mengi hasa ya kuchagua majibu ya kundi fulani la watoto yalifanana ,

“Unakuta katika swali ambalo labda  jibu sahihi lilikuwa ni C unaweza ukakuta wote wamepata kwa kujaza C na mahali ambapo jibu ni E wanafunzi wote ambao matokeo ya yamefutwa waliandika jibu la E,hii haimanishi waliiba kwa sababu inawezekana walijua jibu ni E lakini kuna swali ambalo  jibu sahihi ni B wanafunzi wote waliofutiwa matokeo walikosa swali hilo ambapo wote walikosa kwa kujaza jibu  A ,hapo lazima ujiulize darasa zima waliokosea  wote waliona jibu ni A? ,

“Hili ni moja unaweza ukasema hili linaweza kutokea,ukienda kwenye kipingele kingine jibu ni D wanafunzi wote  waliofutiwa matokeo wao wakaandika ni C inaonyesha yule aliyekuwa anawafundisha majibu naye alikosea akawaambia jibu ni C nao wakaandika C,hii inatosha kukwambia kuna kitu kinaendelea, wanapopata wamepatia sawa wote, lakini hata wanapokosa walikosea kwa namna moja wote ,hii haiwezekani lazima hawa watu wamewekwa mahali wamefundishwa .”

“Ameongeza ‘kwa mfano katika shule ya Pakafa ambayo wazazi waliandamana watahiniwa walikuwa 192 ambayo wanafunzi 140 majibu yanafanana  na ndiyo ambao matokoe yao yamefutwa

hao waliobakia hatujui kama walionyeshwa mtihani lakini waliamua kujibu kwa namna yao wenye hatujui lakini Baraza la mtihani  limeamua kutochukua hatua dhidi yao bila kuwa na sababu za msingi za kuwazuia lakini siyo kwa sababu ni watoto wa vigogo na kumbukumbu zote zipo kwa yeyote atakayekuja kuhitaji ufafanuzi zaidi.”

Akiungumzia shule ya Twibhok ya mkoani Mara Waziri Mkenda amesema wanafunzi waliofanya mitihani walikuwa 67,lakini 66 majibu yao yalifanana kasoro mmoja ambaye majibu yake hakufanana na wenzake na kwamba hakukuwa na sababu za kutosha za kumfutia huyo mmoja mitihani yake.

Hata hivyo amesema,Baraza linaendelea na uchunguzi kwa mfano katika shule hiyo ya Twibhok ,watuhumiwa 12 wapo mahabusu kuna ushahidi wa kutosha wa kuwaweka mahabusu kwamba wamehusika nawizi wa mitihani , uchunguzi wa polisi unaendelea .

Vile amesema,watumishi wote wa Serikali waliosimamia mitihani hiyo kwenye shule zilzoonyesha ubadhirifu ,barua zimeandikwa katika mamlaka zao  za ajira kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri kwenye vyumba vya mitihani .

“Kwa hiyo siyo kwamba matokeo tu yamefutwa lakini uchunguzi bado unaendelea kwa ajili ya hatua zaidi dhidi ya wahusika ,na vituo kama hivi bado NECTA  pia linamalizia litatangaza kilichojiri.

Vile vile amesema,kuna watahiniwa 24 katika kituo na shule ya Cornellius iliyopo Kinondoni Dar es Salaam ambapo amesema katika kituo hicho walifundishwa mtihani ambapo ushahidi upo kwamba waliingizwa kwenye bwalo la chakula wakafundishwa mitihani ndiyo wakaingia kufanya mitihani .

“Polisi na watu wetu wamefanya uchunguzi na nakala za maandishi ya wanafunzi na wahuska waliokiri polisi kwamba walienda kwenye bwalo la chakula na kufundishwa ,kwa hiyo matokeo yamefutwa kituo tayari kimeondolewa katika orodha ya vituo vya mitihani ,maana hatuna haja ya kuwa na kiwanda cha kufundisha udanganyifu wa mitihani .”