November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Mbarawa amtaka Mkandarasi upanuzi wa bandari ya kemondo,Bukoba kuongeza kasi

Na Ashura Jumapili,Bukoba,

Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbalawa amemtaka mkandarasi anayetekekeza mradi wa upanuzi wa bandari za Kemondo na Bukoba zilizopo wilayani Bukoba mkoani Kagera kuongeza Kasi ya ujenzi wa mradi huo ili kufikia mwezi may mwaka

Profesa Mbalawa aliongozana na viongozi mbalimbali kutoka mamulaka ya Bandari Tanzania TPA kutoka wakati wa ziara yake Mkoani Kagera alipofika kukagua upanuzi wa bandari za Bukoba na Kemondo zinazogharimu bilioni 40.

Amesema kuwa amefurahia kuona ujenzi haujasimama unaendelea kwa Kasi ambapo ujenzi wa Gati Moja Kwa Kila bandari unapaswa kukamilika kwa wakati na haraka Sana ifikapo Mei ili kuruhusu meli ya Mv Mwanza kutia nanga pindi itakapokamilika.

Amesema kuwa licha ya kuwa mkataba unaonesha mradi huo kukamilika mwezi julai mwaka 2024 ipo sababu ya mradi huo kukamilika mwezi mei ili meli mpya ya Mv Mwanza inapokamilika iweze kuwa na eneo lake la kutia nanga.

“Serikali haina tatizo la fedha naomba usimamizi ufanyike kwa weledi na kazi ifanyike kwa bidii ili meli tu inapomalizika ya Mv Mwanza na Ujenzi wa Gati uwe umemalizika kwa weledi wa Mamulaka ya Bandari na TPA naamini iko litafanyika na tayari tushaongea na wataalamu wote wanaohusika na jambo hilo,”alisema.

Amesema sehemu ambazo meli inapita vifaa vya usalama na ulinzi ambavyo vinaonesha alama na njia zake vifungwe ili kupunguza changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza Mara kwa Mara katika njia za maji .

Kaimu Mkurugenzi kutoka mamulaka ya Bandari Nchini Mhandisi Juma Kijavara amesema kuwa kwa Sasa ujenzi huo unaendelea vizuri na mkandarasi Yuko tayari kufanya kazi usiku na mchana ili kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati .

Amesema kupitia Mradi huo tayari umezesha watanzania wazawa zaidi ya 200 kupata ajira za kudumu huku wakijiongezea uzoefu wa kufanya kazi katika miradi mingine ya Bandari ambayo unatekelezwa na serikali ya awamu ya sita .