Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameshiriki katika Kambi ya Mabingwa katika Hospitali ya Mkoa Mwanza, Sekou Toure (15/11/2021) kwa kufanya vipimo vya kisasa vya Moyo (Trans Thoracic Echocardiography).
Prof. Makubi ni Daktari bingwa wa Moyo na damu na amebobea katika magonjwa ya Moyo kupanuka na kushindwa kufanya kazi (Heart Failure).
Prof. Makubi Pia Echo-Sonographer (mtalaamu wa kutumia mashine ya vipimo vya Moyo).
Aidha, ametoa wito kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujitokeza zaidi katika huduma hiyo ya bure kutoka kwa Mabingwa wa magonjwa mbalimbali.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba