Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
MAMLAKA ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA)imeutangaza rasmi Mfumo wake mpya wa ununuzi wa Umma wa kielektroni ujulikanao kama NeST ambapo sababu kubwa ya kujengwa kwa Mfumo huo ni kutokana na hitaji la kuhakikisha ununuzi wa Umma unazingatia misingi mikuu ya Kimataifa katika ununuzi wa Umma ambayo ni uwazi pamoja na kuzuia mwenendo mbaya.
Hayo yameelezwa jijini hapa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Dkt.
Leonada Mwagike wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa ununuzi kwa njia ya Mtandao-Nest ambao unatarajiwa kuanza kutumika rasmi Julai Mosi Mwaka huu.
Mwenyekiti huyo ametaja sababu kubwa ya ujenzi wa mfumo wa NeST ni hitaji la kuhakikisha ununuzi wa umma unazingatia misingi Mikuu ya Kimataifa katika ununuzi wa umma ambayo ni uwazi,usimamizi mzuri wafedha za umma,kuzuia mwenendo mbaya,ukidhi na ufuatiliaji na uwajibikaji na Udhibiti.
“Hatua hii pia imezingatia na ongezeko la mahitaji katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA ndani ya sekta,”amesema Mwagike.
Aidha ameeleza kuwa mfumo huo utatumika katika hatua zote za michakato ya ununuzi kuanzia utangazaji wa zabuni mpaka utoaji wa tuzo za zabuni.
“Kwasasa tutaanza na taasisi nunuzi 101 katuka awamu ya kwanza itakayoanza Julai 1,mwaka huu na taasisi nunuzi zilizobaki zitaanza kutumia mfumo huu wa NeST Oktoba 2023 na baada ya hapo taasisi nunuzi zote hazitaruhusiwa kuendesha michakato ya ununuzi nje ya mfumo huo,”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA)Eliakim Maswi ameeleza faida za Mfumo mpya wa NeST.
Ambapo amesema kuwa kuongezeka kwa uwazi kwa kuondoa kwa kiasi kikubwa mwingiliano wa kibinadamu na maamuzi ya kibinadamu,kuongezeka kwa uwajibikaji ambapo mfumo umeweka magawanyo wa majukumu kwa kila mtumiaji na kuweka uwezo wa kufuatilia kila kilichofanyika na hivyo ni rahisi kwa yeyote kuwajibika kwa makosa anayoyafanya wakati wa kufanya ununuzi wa umma.
Pia ametaja faida nyingine kuwa ni kupata huduma zilizo bora pamoja na kuongeza ukidhi wa sheria,kupunguza mianya ya rushwa na upatikanaji wa taarifa kwa jili ya kufanya maamuzi mbalimbali.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato