November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PPRA ilivyoibuka kidedea maonesho 77

Na Joyce Kasiki, Timesmajira online DarĀ 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA),imeshinda tuzo ya mshindi wa kwanza katika kipengele cha mamalaka za uthibiti.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Eliakim Maswi,Ā  katika banda Lao mara baada ya kupokeaĀ  tuzo ya mshindi wa kwanzaĀ upande wa Mamlaka za Udhibiti kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (SabaSaba)Ā  Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Pwani Vicky Mollel amesema ushindi huo unaenda kuongeza chachu ua utendaji kazi wao.

Amesema,pia ni furaha kwao kwa kuhudumia watu wengi kwenye banda lao huku akisema makadirio yao ilikuwa ni watu 500 lakini wameweza kuhudumia watu zaid ya 700.

Amewataka  wananchi Taasisi za Umma na sekta binafisi  kujiandaa kutumia Mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma wa kielektroniki (NeST), kwa ajili ya michakato ya ununuzi wa Umma.

 Mollel amesema, katika Sheria ya manunuzi ya Umma namba 10 ya mwaka 2023 kuna fursa nyingi kwa ajili ya Watanzania wajiandae kushiki fursa hizo ili kukuza uchumi wa Tanzania.

“Tuna shukuru kwa mafanikio haya makubwa  ambayo tuyapata katika maonesho haya kama PPRA tulijipanga kutoa elimu kwa ajili ya matumizi ya Mfumo wa NeST kutokana na Sheria mpya ya manunuzi ya Umma,” amesema.

Amesema  kuwa mamlaka hiyo ilitarajia ushindi kutokana na nguvu kubwa waliyoiweka katika kuhamasisha Umma na kwamba walihakikisha banda hilo linakuwa zuri la kuvutia wateja kupata huduma.

Mollel amefafanua kuwa siri ya mafanikio ya PPRA ni kufanya kazi kwa pamoja  kama timu na kuweza  kujituma.

Aidha amewataka wananchi wanaposikia maonesho wawe wanatembelea kwa kuwa kuna vitu vizuri yanayoandaliwa na PPRA kwa ajili ya wateja wao.

Meneja huyo ameeleza kuwa baada ya kupata tuzo hiyo watakuwa na msukumo makubwa wa kutoa huduma kwa wateja wao ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa lengo la kuwafikia wateja zaidi hao